| Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam katikati ni mratibu wa mpambano uko kochwa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| Mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| Bondia Mada Maugo akikabiziwa mkataba wake na mratibu wa mapambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kati yake na Abdallah Pazi mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea sehemu ya fedha yake kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa anaetoa fedha hizo ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS |
| Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea mkataba wake kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kusaini kwa ajili ya kupigana na Mada Maugo siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano wa raundi nane KG 76.
Akizungumza wakati wa kutiliana saini mikataba hiyo kocha wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano uho
Amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo ambao wanatamba katika tasnia ya masumbwi nchini ili wapenzi wa mchezo wa masubwi waburudike siku hiyo ya sikukuu ya pasaka
Mbali na mpambano uho siku hiyo bondia chipkizi anaekuja kwa kasi zaidi katika mchezo wa masumbwi Vicent Mbilinyi anaetokea katika Super D Boxing Promotion atakae pambana na Mwinyi Mzengela mpambano wa KG 63 raundi nane mpambano mwingine utawakutanisha bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba
Siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni