.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 9 Februari 2016

MTANZANIA AUWAWA KWENYE KAMARI KENYA BAADA YA KUWASHAMBULIA MAMENEJA WA CASINO


Mcheza kamari mmoja anayedaiwa kuwa ni raia wa Tanzania amepandwa na hasira na kuwakata kwa panga mameneja wawili wa Casino baada ya kucheza kamari na kuliwa shilingi 30,000 za Kenya huko Eastleigh, Nairobi.

Mcheza kamari huyo John Muchanga hata hivyo alidhibitiwa na kisha kuuwawa na watu wenye hasira alipokuwa akijaribu kumshambulia meneja wa tatu kwenye casino ya City View iliyopo barabara ya Tenth.

Mkuu wa polisi Jijini Nairobi Japheth Koome amesema Muchanga alimfuata meneja mwanamke akimtaka amkopeshe fedha za kucheza kamari baada ya kuliwa na aliponyimwa alitoka nje na kuja na panga na kuanza kumshambulia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni