Polisi katika Jiji la Moscow nchini
Urusi wanamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumuua mtoto baada
ya kukutwa akiwa amebeba kichwa kilichokatwa cha mtoto huyo.
Mwanamke huyo anayedhaniwa kuwa ni
mtumishi wa ndani anatuhumiwa kumuua mtoto huyo na kisha kuchoma moto
nyumba ya wazazi wa mtoto huyo.
Picha za CCTV zimemuonyesha mwanamke
huyo aliyevalia hijabu, akitembea karibu na usafiri wa treni akiwa
ameshikilia kichwa cha mtoto.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni