Sheha wa Shehia ya Kilimani akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitowa maelezo ya eneo mpja lililoathirika na Tabia nchi katika eneo la kilimani akimuonesha uliokuwa uwanja wa kilimani Stars kwa sasa uwanja huo umekuwa ni sehemu ya kukaa maji ya bahari wakati wa maji kujaa. na kufika karibu na sehemu ya makaazi ya wananchi.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitembelea eneo hilo wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Tabianchi Zanzibar akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakiwa kastika ufukwe wa pwani ya kizingo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina na Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nadi Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni wakitembelea eneo la ufukwe wa pwani ya kilimani ilioathirika kwa kuliwa na bahari sehemu kubwa ya eneo hilo na kuingia maji katika maeneo ya jirani na makaazi.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kudhibiti tabia nchi kwa eneo hilo la kilimani na kuharibu sehemu kubwa ya eneo hilo ambalo lilikuwa na uwanja wa mpira na kuliwa na bahari.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo hilo lililokubwa na athari za Tabia nchi katika pwani ya ufukwe wa kilimani na kuagiza kupandwa kwa mikoko katika eneo hilo ambolo ifikapo mwezi wa marchi na fedha zake zipo kwa kazi hiyo na zoezi hilo limeaza mwezi huo kwa kuaza kwa kupandwa kwa miti ya mikoko na ujengaji wa tuta la kuzuiya maji ya bahari kuendelea kula eneo hilo ambalo tayari limeharibia na maji ya bahari.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina Naibu Waziri wa Mambi ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mbunge wa Jimbo la Jangombe Mhe. Ali Hassan Omar King wakitembelea eneo la pwani ya kilimani lililokumbwa na athari za TabiaNchi. wakati wa ziara yake Kisiwani Zanzibar kutembelea maeneo hayo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
Zanzinews.com.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni