Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir
amemteuwa tena mpinzani wake aliyekuwa muasi Riek Machar kuwa Makamu
wa Rais wa taifa hilo changa la Afrika kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na televisheni ya taifa hilo.
Uteuzi huyo wa Machar uliotangazwa
na televisheni ya taifa unachukuliwa kuwa ni sehemu ya makubaliano ya
amani yanayolenga kumaliza machafuko yaliyoduma kwa muda wa miaka
miwili.
Sudani Kusini imekuwa katika
machafuko tangu Desemba 2013, wakati mapigano kuibuka baina ya vikosi
vitiifu kwa Kiir na wanajeshi wanaomuunga mkono Riek Machar, ambaye
awali alikuwa makamu wa rais.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni