Wabunge wa upinzani nchini Afrika
Kusini wametolewa nje ya bunge wakati rais Jacob Zuma akilihutubia
taifa kupitia bunge kutokana na kumkatiza mara kwa mara asihutubie.
Kiongozi wa wabunge wa chama cha
mrengo wa kushoto cha Wapigania Uhuru wa Uchumi, amesema rais Zuma
amelifanya taifa kuonekana ni mzaha.
Hotuba hiyo ilionekana kama ni
sehemu ya rais Zuma, kupotezea kesi inayomkabili ya kutumia dola
milioni 23 za umma kukarabati nyumba yake.
Kambi ya upinzani imekata uamuzi wa
rais Zuma, kurejesha fedha hizo zilizotumika kwa ujenzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni