.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 10 Februari 2016

WAZAZI KISARAWE WAFUNGUKA KUHUSU ADHABU KWA WATOTO

Joseph Olowa akiiomba kampuni ya True Vision kusaidia kuelimisha watu wenye lugha za matusi hadharani hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Mtoto akionesha jeraha alilopata baada ya kuchapwa na baba yake alipokuwa mdogo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Mkazi wa kisarawe Juma Athumani akitoa ushuhuda wa adhabu ya kufukuza watoto nyumbani hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.
Cornel Anatory akielezea alivyomwagiwa maji ya ugali utotoni hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Hamisi Idd akihamamisha wazazi kuwapa watoto elimu ya dini tangu utotoni ili kuepuka tabia mbaya hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Jamila Shabani akisema kuwa moja ya adhabu wanayopewa watoto ni kuchapwa fimbo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Kimela Billa Mtayarishaji wa vipindi vya Walinde Watoto akikabidhi Redio kwa Bi. Mwashamba Mrisho ambae ni mtendaji kata wa kata ya Kibo   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Kikundi cha Kisarawe Bomani maarufu kama Kibo katika picha ya pamoja baada ya kupata redio kutoka True Vision hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Kikundi cha Tushirikiane cha Kisarawe wakijadiliana baada ya kupewa Redio na True Vision ili kufuatilia vipindi vya Walinde Watoto hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

                                                                             Na Krantz Mwantepele , Kisarawe 

Watanzania wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga urafiki nao ili kuwawekea misingi bora ya nidhamu na upendo. Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wazazi na walezi kutoka wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.

Katika mdahalo huo mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo athari za kuchapa watoto, matusi pamoja na adhabu kali kwa watoto mfano kuwafukuza watoto nyumbani.

Aidha washiriki wa mdahalo huo walionyesha kusikitishwa na vitendo vya kuchapa watoto fimbo kupita kiasi na wengine wakikemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kutukana watoto pasipo kuzingatia maadili huku wakiiomba serikali kuwawajibisha wale wote wanaotukana hadharani bila kujali uwepo wa watoto.

Katika hatua nyingine, washiriki hao walikemea tabia ya kuwafukuza watoto nyumbani na kudai kuwa huo ni mwanzo wa kuwaingiza watoto katika matatizo makubwa na kuongeza idadi ya watoto wa mitaani aidha wamependekeza kuwa ni vyema watoto wafanyiwe maombi mara kwa mara na kuwashirikisha katika Ibada ili kuwaepusha kuwa na utovu wa nidhamu.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Kibasila Kisarawe ambao walipata nafasi ya kuongea na timu ya Walinde Watoto walionyesha kuchukizwa na tabia ya kupewa adhabu kupita kiasi pamoja na kutukanwa tabia ambayo hufanywa na baadhi ya walimu na wazazi.


Naye mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibasila Kisarawe Debora Mbalilaki alipendekeza kuangalia uwezekano wa kuwepo na adhabu mbadala badala ya fimbo kwa wanafunzi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni