Ndege ya EasyJet iliyokuwa ikitokea Geneva imelazimika kusita
kuruka dakika chache kabla ya kuanza kuondoka baada ya mmoja wa
abiria kuona spana kwenye bawa la ndege.
Ndege hiyo ya abiria ilishakuwa imeruhusiwa kuanza kuelekea
kwenye njia ya kupaa, ndipo abiria mmoja raia wa Uswizi alipoona
spana na kuwaarifu wahudumu wa ndege.
Rubani wa ndege ilibidi airejeshe ndege katika eneo la maegesho
na spana hiyo kuondolewa, ambapo uchunguzi umeanza kufanywa juu ya
tukio hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni