Kikosi cha Mbeya City Fc tayari kipo jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya African Sports unaotajia kuchezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mapema leo mkuu wa kitengo cha utabibu kikosi Dr Joshua Kaseko amesibitisha kuwa wachezaji wote 18 walisafiri kutoka jijini Mbeya tayari wa mchezo huo wako kwenye hali nzuri kabisa na ana imani kubwa watacheza kwenye kiwango bora ili kuipatia matokeo timu yao hapo kesho.
“Joseph Mahundi alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, hivi sasa yuko vizuri na tunatarajia atakuwa sehemu ya kikosi hapo kesho, hakuna shaka kuwa City iko hapa Tanga kwa sababu ya kupata matokeo na hakuna jambo lingine, tumetoka kushinda dhidi ya Stand United jambo linalotupa nguvu ya kupambana hapo kesho, tuna morali ya hali ya juu kikosini ambapo kila mmoja ana hamu ya kurudi na pointi tatu” alisema.
Kwa upande wake Kocha Kinnah Phiri ameweka wazi kuwa japo hali ya hewa ya hapa ni tofauti kabisa na ile iliyopo jijini Mbeya lakini hiyo siyo sababu ya City kukosa ushindi hapo kesho
“Hali ya hewa ya hapa ni tofauti sana na iliyopo jijini Mbeya, hilo hatulitizami sana, tumejiandaa vya kutosha, asubuhi ya leo tumemaliza mazoezi na wachezaji wamepewa muda wa kuweka miili yao sawa kwa kuoga kwenye barafu, hakuna shaka yeyote kuwa tunazo pointi tatu kutoka hapa” alisema.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni