Dereva wa mbio za Langalanga
Fernando Alonso amenusurika kifo kimiujiza baada yakupata ajali
katika mbio za Australian Grand Prix na gari lake kuharibika vibaya
baada ya kugongwa na Esteban Gutierrez katika mzunguko wa 18.
Gari la Alonso likijibamiza kwenye uzio wa ukuta baada ya kugongwa
Fernando Alonso akitoka kwenye gari lililoteketea baada ya kupata ajali
Katika mbio hizo Nico Rosberg wa
Mercedes alifanikiwa kutwaa nafasi ya kwanza, bingwa wa dunia wa mbio
hizo Lewis Hamilton naye wa Mercedes alishika nafasi ya pili na
nafasi ya tatu ilitwaliwa na Sebastian Vettel wa Ferrari.
Lewis Hamilton akimwagia Champagne usoni Nico Rosberg huku Sebastian Vettel akiangalia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni