Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa amejikuta katika utata wa
tukio la kumng'ata mchezaji wa Everton, wakati Romelu Lukaku
akiyayusha ndoto za Chelsea za kutwaa kombe lolote msimu huu baada ya
kufunga magoli mawili yaliyoitoa kwenye michuano ya kombe la FA.
Diego Costa alionekana akigusisha mdomo wake kwenye shingo ya
mchezaji wa Everton Gareth Barry wakati walipokuwa wakigombana na
kumpelekea Costa kupatiwa kadi nyekundu ya kwanza tangu ahamie
kucheza nchini Uingereza.
Costa mwenyewe amekanusha kumg'ata Barry, na hata mwisho wa
mchezo huo makocha wote wa timu hizo Guus Hiddink na Roberto Martinez
walisita kutoa tuhuma kwa mshambuliaji Diego Costa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni