Mchezaji wa West Ham Dimitri Payet
na kiungo wa Leicester City N'Golo Kante wote wamefunga goli katika
siku yao ya kuzaliwa jana na kuisaidia Ufaransa kuifunga Urusi mabao
4-2 katika dimba la Stade de France.
Katika mchezo huo wa kwanza
kufanyika katika dimba hilo tangu mashambulisi ya Paris, Kante
alifunga goli la mapema kabla ya Andre-Pierre Gignac kuongeza la
pili. Alexander Kokorin alisawazisha bao moja kabla ya Payet kufunga
kwa mpira wa adhabu wa umbali wa yadi 30.
Urusi ilijitutumua na kufunga bao la
pili kupitia Yuri Zhirkov lakini Payet alimtengenezea pande
Kingsley Coman na kupachika bao la nne katika dakika za mwisho.
N'Golo Kante akishangilia goli alilopachika
Kingsley Coman akipachika bao la nne la Ufaransa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni