Na Mwandishi Wetu
Bondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo mkoa wa Pwani ametoa onyo kali kwa bondia Seba Temba kutoka Morogoro kuwa yeye sio njia ya kupita kwa kuwafuata mabondia wa juu hivyo atahakikisha anamsambalatisha Temba.
Akiongea kwa njia ya simu kutoka Bagamoyo Pialali amesema, "nimesikia Temba anatamba kuwa atanisambalatisha hivyo kauli yake hiyo aifute mara moja kwa kuwa nitampiga kipigo cha mbwa mwizi kwani nimejipanga kuitangaza ngumi mkoa wa Pwani kwani mabondia wote niliocheza nao walichezea kichapo.
Mbali na mpambano huo, siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mengi ya mchezo wa ngumi likiwemo la wanawake Joyce Awino kg 64 na Mariam Tembo na Abdallah Pazi kg 76 atakumbana na Georger Dimoso na Flank Lampad kg 69 atavaana na Mwaite Juma wakati bondia kutoka mkoa wa Tanga Jacobo Mganga kg 72 atapambana na Maono Ally.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na kuuzwa kwa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria za mchezi huo zikiwa na mabondia wakali akiwemo Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine weng.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni