.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 26 Machi 2016

JOHAN CRUFFY AKUMBUKWA KWENYE MCHEZO WA UHOLANZI NA UFARANSA

Mchezo wa kirafiki baina ya Uholanzi na Ufaransa ulisimama katika dakika ya 14 na kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezaji maarufu wa nchi hiyo Johan Cruyff aliyefariki dunia.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Ajax na Barcelona, ambaye alikuwa maarufu akivalia fulana namba 14 mgongoni, alifariki kwa ugonjwa wa saratani Alhamisi, akiwa na umri wa miaka 68.

Katika mchezo huo Uholanzi ilibidi wapambane kiume wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza na kusawazisha baadaye hata hivyo Blaise Matuidi aliipatia Ufaransa bao la tatu katika dakika za mwisho na kufanya matokeo kuwa 3-2.
    Olivier Giroud akiachia mkwaju uliojaa wavuni na kuandika bao la pili la Ufaransa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni