.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Machi 2016

KAMPUNI YA NIKE YAMTOSA MCHEZA TENESI MARIA SHARAPOVA

Kampuni ya Nike imesitisha udhamini kwa Maria Sharapova saa kadhaa baada ya kukiri kutumia dawa za kututumua misuli zilizopigwa marufuku katika michuano ya wazi ya Australia mwezi januari.

Mshindi huyo wa Grand Slam mara tano amebainisha kutenda kosa hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika hoteli Jijini Los Angeles, akikiri kuwa amenaswa na chombo cha kupinga matumizi ya dawa hizo katika mchezo wa tenesi.

Mchezaji tenesi huyo anayelipwa mno kuliko wachezaji mwingine yoyote mwanamke katika mchezo huo, amebainika kutumia dawa aina ya Mildronate ama Meldonium, ambayo ilipigwa marufuku Januari mosi mwaka huu.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni