Shirika Amnesty International
limeishutumu Qatar kwa kuwalazimisha kwa nguvu wafanyakazi wanaofanya
kazi za ujenzi wa maandalizi ya michuano ya kombe la dunia mwaka
2022.
Shirika hilo limesema wafanyakazi wa
uwanja wa mpira wa Kimataifa wa Khalifa wanalazimishwa kuishi kwenye
mazingira duni, kulipa ada kubwa ya kuomba kazi, mishahara yao pamoja
na hati zao za kusafiria ikizuiliwa.
Shirika la Amnesty International
limelishutumu Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa kushindwa kuzuia
maandalizi ya michuano hiyo kufanyika kwa gharama za ukiukwaji wa
haki za binadamu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni