Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akitoa maelezo kabla ya kumuapisha Spika mteule Mhe Zuberi Ali Maulid kwa kushinda katika uchaguzi huo kwa kura nyingi. zilizopigwa na Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk Yahya Khamis Hamad akimuapisha Spika Mpya wa Baraza la Tisa Mhe Zuberi Ali Maulid baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo ili kuliongoza Baraza la Wawakilishi kwa Kipindi cha Miaka Mitano.
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akikata utepe Katiba ya Zanzinar na Tanzania na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha.
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid akitoa shukrani kwa Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi kwa kumpigia Kura kuweza kuliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano.
Makamu wa Pili wa Rais Mteule na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe Balozi Seif Ali Iddi na wajumbe wengine wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani zake na kuahidi ushirikiano na Wajumbe wa Baraza katika Kazi zake za Vikao vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani zake kwa Wajumbe hao baada ya kumpa ushindi wa kishindo.
Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad akiwa na wasaidizi wake katika ukumbi wa mkutano wakati Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani kwa Wajumbe wa Baraza. Kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni