Mtu anayetuhumiwa kuiteka ndege ya
shirika la ndege la Misri na kuilazimisha kutua Cyprus amefikishwa
mahakamani hii leo ambapo polisi imeomba akae rumande kwa siku nane.
Mtuhumiwa huyo Seif al-Din Mohamed
Mostafa, 58, raia wa Misri ambaye mke wake aliyetengananae ni raia wa
Cyprus, hakutakiwa kuzungumza neno lolote mahakamani hii leo.
Mostafa hatofunguliwa shtaka lolote
kwa sasa hadi hapo kesi yake itakapotajwa baadaye na kupewa fursa ya
kujitetea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni