Mtu asiye na makazi huko San
Francisco nchini Marekani atazawadiwa donge nono la dola 100,000 kwa
kuwasaidia polisi kuwakamata wafungwa wawili waliotoroka jela.
Mtu huyo Matthew Hay-Chapman alikuwa
ameziona picha za wafungwa hao wawili kwenye taarifa ya habari, na
kisha baadae kuwaona wakiwa ndani ya gari lililoibiwa.
Wafungwa hao walivunja gereza la
kaunti ya Orange siku sita zilizopita, na kusababisha kuanzishwa
msako mkali wa kutafutwa na vyombo vya dola.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni