Mwanamke amesafiri kwa ndege kutoka Instanbul hadi Paris akiwa
na mtoto wakike wa miaka minne aliyefichwa kwenye begi, shirika la
ndege la Ufaransa limesema.
Shirika hilo la ndege limesema mtoto huyo aliyesafiri bila
tiketi alibainika akiwa ndani ya ndege siku ya jumatatu usiku.
Vyanzo katika uwanja wa ndege vimesema mwanamke aliyefanya
kitendo hicho ni Mfaransa ambaye alikuwa katika mchakato wa kumuasili
mtoto huyo raia wa Haiti.
Shirika la ndege la Ufaransa liliziarifu mamlaka za Ufaransa
lakini waendesha mashtaka wameamua kutomfungulia mashtaka mwanamke
huyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni