Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adelm Meru kwa Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara baada ya Rais huyo kuwasili Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa ajili ya kutembelea Mamlaka hiyo la uwekezaji na kujionea shughuli zinazofanywa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mhe. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akimwelezea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Halotel kutoka nchini Vietnam, ambapo alimwonyesha Vocha za muda wa maongezi za mtandao huo ambazo zinapatikana katika gharama tofauti kulingana na nafasi ya kifedha ya mtumiaji.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong akiongea na viongozi wa Serikali ya Tanzani na Vietnam pamoja na wafanyabiashara katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi za EPZA. Mhe. Truong alieleza kuwa Serikali ya Tanzania ijiandae kupokea wawekezaji wengi zaidi wa Kampuni ya Halotel kutoka nchini kwake kupitia fursa za uwekezaji zilizopo katika kituo cha Uwekezaji cha EPZA .
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni