Miongoni mwa majukumu ya Mwenyekiti wa Mwenzi ni pamoja na kuitisha , kuratibu na kuendesha mikutano inayowahusisha Wawakilishi wa Kudumu kutoka Nchi 53 wanaoziwakilisha Nchi zao katika Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti wa mwezi, pamoja na kuratibu na kuendesha mikutano yenye ajenda mbali mbali pia anawajibika katika kuwasilisha kauli ya nchi za Afrika kupitia ama utoaji wa hotuba au mawasilianona Wakuu wa Idara mbali mbali ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pale inapolazimu.
Pichani ni baadhi ya Matukio yaliyotokea mwishoni wa wiki wakati wa Mkutano wa Wawakilishi hao wa Nchi za Afrika chini ya uenyekiti wa Tanzania, ambapo walipokea taarifa mbali mbali kutoka kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na taarifa kutoka kwa Muungano wa Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Afrika waliokuwa wakishiriki katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa akitoaa raarifa fupi kwa niaba ya Wakurungezi Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Nchi za Afrika kuhusu maazimio na mapendekezo yao kuhusu viashiria vya ajenda ya Maendeleo Endelevu. Kulia kwa Balozi Tuvako Manongi ambaye Tanzania ni Mwenyekiti wa Mwezi wa nchi za Kundi la Afrika ( African Group) Ni Mtakwimu Mkuu kutoka Ivory Coast.
Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa, Bw. Taye-Brook Zerihoun naye akiwasilisha taarifa yake kwa Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wawakilishi hao kuunga mkono pendekezo la Idara yake la kupatiwa fedha ambazo wanataka kuzitumia katika eneo la uratibu na usimamia wa majadiliano kuhudu dhana nzima ya uzuiaji wa machafuko ( mediation and prevention ) pamoja na kuongeza ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa UN-Women Phumzile Mlabo Ngcuka akiwaeleza Mabalozi kuhusu mkutano wa 68 wa Kamishini Juu ya Hali ya Wanawake utakaoza siku ya Jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,Mada kuu ya Mkutano wa mwaka huu ambao huwakusanya mamia ya viongozi wanawake kutoka mataifa yote duniani ni Uwezezaji wa Wanawake kupitia utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( aganda 2030) Kushoto wa Balozi Manongi ni Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataita, Balozi Antonio Tete
Sehemu ya Mabalozi na Maafisa kutoka nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika wakifuatilia mkutano.
Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi zawadi ya kumuanga kwa niaba ya Mabalozi wenzie aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Marjon V. Kamara ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Liberia.
Kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni