.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Machi 2016

UJUMBE WA JWTZ WATEMBELEA UBALOZI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WASHINGTON, DC

Pichani kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda

Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kikeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. 

Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni