.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 9 Machi 2016

WAANDISHI WA HABARI WAMEASWA KUANDIKA HABARI ZENYE TIJA KWA TAIFA

MNG1
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali kifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
MNG2
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Victoria Msina akimkaribisha Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
MNG3
Baadhi ya washiriki wa semina wakimskiliza Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
MNG4
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
MNG5
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.

                                                                                       Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Wanahabari nchini wameaswa kutumia taaluma yao vema katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya uchumi, biashara na fedha kwa lugha ambayo wananchi wa ngazi mbalimbali wataweza kuelewa kirahisi ili waweze kuchangia katika maendeleo yenye tija kwa taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta ya uchumi na fedha.

“Benki Kuu ya Tanzania inatambua na inathamini sana mchango mkubwa unaofanywa na magazeti, vituo vya televisheni na radio kwa kutenga nafasi maalum kwa ajili ya habari za fedha na uchumi na hasa zinatolewa na Benki Kuu” alisema Bw. Richard.

Katika kuhakikisha vyombo vya habari vinatoa elimu katika masuala ya fedha na uchumi, Bw. Richard amesema kuwa BoT imechukua jukumu la kuwajengea uwezo wanahabari kila mwaka ili kuwaongezea uelewa wao kuhusu majukumu na kazi za Benki hiyo na mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Malengo mengine ya semina hiyo ni kuchochea na kukuza ari ya wanahabari katika kuandika habari za uchumi na fedha, kutafsiri na kuchambua taarifa mbalimbali za uchumi na fedha zinazotolewa na taasisi mbalimbali, kuwafahamisha wanahabari masuala yanayoendelea katika uchumi wa Tanzania na wa dunia, mwelekeo wa uchumi na masuala ya fedha katika siku zijazo na kuimarisha uhusiano mzuri wa kikazi uliopo baina ya vyombo vya habari, wanahabari na Benki Kuu.

Zaidi ya hayo, Bw. Richard ameongeza kuwa Benki Kuu kama taasisi, inajukumu la kujifunza namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi na mahitaji yao katika kuandaa na kuwasilisha taarifa na habari za uchumi na fedha.

Aidha, Bw. Richard amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini unaoendelea sasa unatokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali na BoT katika kutekeleza sera za uchumi na fedha pamoja na usimamizi wa uhakika wa sera hizo.

“Kadiri uchumi unavyokua na kadiri mazingira ya biashara yanavyoendelea kuvutia wawekezaji, mahitaji ya taarifa na habari sahihi na kwa wakati kuhusu uchumi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na masoko ya fedha, uchumi wa kanda na dunia kwa ujumla yanaongezeka sambamba na umuhimu wake” alisisitiza Bw. Richard.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa semina hiyo kwa niaba ya wanahabari hao Ezekiel Kimwaga kutoka gazeti la Raia Mwema ameupongeza uongozi wa BoT kwa kufikisha miaka 50 na kuishukuru benki hiyo kuthamini na kutoa fursa ya semina hiyo kwa wanahabari kila mwaka ambayo inawaongezea uelewa katika masuala ya uchumi na fedha.

Semina hiyo ya siku nne inajumuisha mada mbalimbali zinazowasilishwa na wataalam kutoka BoT ni pamoja na kuzijua kurugenzi ambazo zinazohusika na masuala ya uchumi, biashara na fedha ambazo ni Utafiti na Sera za Uchumi, Masoko ya Fedha, Usimamizi wa Mabenki, Bodi ya Bima na Amana, Mifumo ya Malipo ya Taifa na Huduma za Kibenki.

Mada nyingine katka semina hiyo ni kuzijua alama za usalama zilizopo katika fedha, dawati la malalamiko ya wateja wa mabenki pamoja na kuzijua kazi za matawi ya Benki Kuu ya Tanzania.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni