Mamia ya wahamiaji waliokwama katika kambi Ugiriki
wanahatarisha maisha yao kwa kukatiza mto wenye maji katika kujaribu
kuingia Ulaya.
Njia hiyo hatari tayari imechukua maisha ya wakimbizi watatu
akiwemo mwanamke mjamzito ambaye mwili wake umeibuliwa kutoka majini
karibu na mpaka wa Macedonia hii leo.
Lakini saa chache baadaye wahamiaji wengine wapatao 1,000
wakiwemo wanawake, watoto na hata mtu mlemavu aliye kwenye kiti cha
magurudumu walikuwa wakijaribu kukatiza mto huo baada ya kuelezwa
hakuna uzio katika upande wa pili.
Mwanamke akisaidiwa kuvuka kwenye mtu huo na wahamiaji wenzake
Ni safari hatari lakini yenye matumaini ya kuingia Ulaya na kupata maisha bora kwa wahamiaji hawa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni