Timu ya Barcelona inayojianda na
mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Ulaya dhidi ya Arsenal hii leo,
imeonekana haina mchecheto na mechi hiyo baada ya jana kupata muda wa
kucheza na watoto wawili waliovamia uwanjani wakati wa mazoezi yao.
Ikiwa tayari imeshaielekeza kibla
timu ya Arsenal kwa mabao 2-0, katika mchezo wao wa kwanza katika
dimba la Emirates, wachezaji wa Barcelona wanajiandaa kuichinja
Arsenal leo usiku katika dimba la nyumbani Nou Camp.
Watoto waliovamia mazoezi ya Barcelona wakiwa na Lionel Messi
Neymar akimpiga picha mmoja wa watoto hao akiwa na Luis Suarez
Dogo pia alipata muda wa kucheza mazoezi na wachezaji wa Barcelona




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni