.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 11 Machi 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE AMEITAKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KUTOA MAFAO KWA WAKATI

SAM_7871
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane wa wadau wa LAPF unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo alikuwa mgeni rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili kuhakikisha kuwa wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
SAM_7793
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi
SAM_7774
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha
SAM_7761
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha
SAM_7811
Afisa Masoko wa LPF James Mlowe akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari mfuko huo umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF ambao unalenga kuwasaidia watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa maeneo ya vijijini ili waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania bila vikwazo vya kiuchumi…


SAM_7828
Makamu mwenyekiti wa bodi Husein Kamote alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha utekelezaji wa mipango yake ikiwemo deni inalolidai serikali ambalo halijalipwa kwa mda mrefu huku likizidi kuongezeka
SAM_7803
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga
SAM_7758
Wadau katika mkutano
SAM_7817
Mdau kutoka benki ya NMB akizungumza katika mkutano huo
SAM_7866
Mwandishi wa habari wa star tv  Ramadhan Mvungi akifatilia mkutano kwa ukaribu
SAM_7859
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
SAM_7858
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
SAM_7855
Waziri wa TAMISEMI George Simbachaweneakimkabidhi kaimu mkurugenzi Geita John Muta hundi ya shilingi milioni saba tu baada ya halmashauri hiyo kufanya vizuri na mfuko huo
SAM_7765
Wadau wakifatilia mkutano
SAM_7783
Wadau kutoka mifuko mingine pia walishiriki mkutano huo
SAM_7826
Mnufaika wa LAPF kupitia maisha popote Scolastika Francis kutoka Kilolo ambaye ni mwalimu akitoa ushuhuda jinsi mkopo huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo sasa anamiliki nyumba pamoja na shamba mbali na ajira yake
SAM_7823
Mwalimu wa shule ya sekondari Rombo Njuguna Rombo akitoa ushuhuda jin si mfuko huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo ameweza kununua kiwanja huku akimiliki mradi wake wa kuku

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni