Mchezaji Gabriel Agbonlahor
hatoichezea Aston Villa wakati klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza
ikifanya uchunguzi kuhusiana na tabia yake.
Mshambuliaji huyo amenaswa kwenye
picha akivuta shisha akiwa mapumzikoni nchini Dubai wakati wa
mapumziko ya mechi za kimataifa.
Kufuatia uchunguzi huo Agbonlahor,
29, atakosa mchezo wa jumamosi dhidi ya Chelsea utakaochezwa kwenye
dimba la Villa Park.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni