.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Aprili 2016

BARCELONA YAZINDUKA NA KUICHAKAZA DEPORTIVO LA CORUNA

Timu ya Barcelona imeibuka kwa kasi kutoka usingizini baada ya kuchezea vichapo katika mechi tatu za nyuma za La Liga na kuichakaza Deportivo La Coruna kwa magoli 8-0.

Katika mchezo huo Luis Suarez alifunga magoli manne, Rakitic kuongeza la tano, Messi akafunga la sita, Bartra akatumbukiza la saba kabla ya Neymar hajakamilisha la nane.
                                                                    Luis Suarez akifunga goli la kwanza 
                 Neymar akimchambua kipa wa deportivo la Coruna na kupachika goli
Nayo Real Real Madrid imeendelea kuzifukuzia kileleni Barcelona na Atletico Madrid latika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal kwenye dimba la Bernabeu.

Goli la kichwa la Karim Benzema liliifanya Real Madrid iongoze katika kipindi cha kwanza, na katika kipindi cha pili Lucas Vazquez akafunga la pili kabla ya Luka Modric kuhitimisha la tatu, na kuipa Real Madrid ushindi wa nane mfululizo.
                                                 Benzema akipachika goli kwa mpira wa kichwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni