Kocha mkuu wa Mbeya City fc Kinnah Phiri ametangaza orodha ya nyota
18 watakao kuwa sehemu ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopangwa kuchezwa jumamosi hii
Manungu Complex , Turiani, Morogoro.
Akizungunza na Mbeya City Fc muda mfupi baada ya kumalizika kwa
mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Kocha Phiri
alisema kuwa hana tatizo na nafasi ya 10 iliyopo timu yake hivi sasa
kwenye msimamo wa ligi kwa sababu anaamini ushindi kwenye michezo miwili
ijayo utakifanya kikosi chake kusogea mpaka nafasi ya 8.
“Msimamo wa ligi unaonyesha tuko kwenye nafasi ya 10,
hili siyo tatizo sana kwa sababu kushinda mechi mbili zijazo
kutatuingiza kwenye timu nane bora, hili ndiyo lengo letu, tunayo
michezo minne mbele nina uhakika kwamba kila mchezaji anafahamu kuwa
tunatakiwa kuongeza pointi zaidi ili tumelize ligi tukiwa sehemu ya timu
nane za juu” alisema.
Akiendelea zaidi Kocha Phiri alisema kuwa kwenye mchezo huo wa
morogoro kikosini atawakosa nyota kama Raphael Daud anayeguza majereha
ya mguu pia mlinzi Haruna Shamte aliyekwenye zuio la kucheza kufuatia
kadi za njano, huku pia akiwakosa Haruna Moshi Boban na nahodha Temi
Felix ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo
ya kifamilia.
“Ni wazi hatutakuwa na Haruna Moshi Boban anayesumbuliwa
na maralia, pia tunamkosa Temi, tunafahamu alikuwa nje ya timu
akishughulikia masuala ya kifamilia amerudi kambini juzi hivyo kwa
vyovyote hawezikuwa sehemu ya mchezo huo, Rahael Daud ni mgonjwa na
Haruna Shamte ana zuio la kadi za njano, kutokuwepo kwao hakuondoi
dhamira yetu ya kushinda mchezo kwa sababu tumekuwa namaandalizi mazuri
na muhimu kwa wachezaji wetu wengine ambao sasa wako tayari” … alimaliza Kocha Phiri na kutaja baadhi ya nyota wakaosafiri tayari kwa kuivaa Mtibwa Sugar jumamosi hii.
Miongoni mwa nyota ambao kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya
Malawi aliwataja ni pamoja na Juma Kaseja, Haningtony
Kalyesubhula,John Jerome, John Kabanda,Yusuph Abdalah,Deo Julius, Tumba
Lui,Hassan Mwasapili, Kenny Ally, Hamidu Mohamed, na Meshack Samwel na
kusema kikosi chake kinataraji kuanza safari jioni ya leo moja kwa
moja kuelekea wilayani Turiani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni