.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 8 Aprili 2016

DIVOCK ORIGI AIPATIA LIVERPOOL GOLI MUHIMU UGENINI

Mshambuliaji Divock Origi ameipatia Liverpool goli muhimu katika mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Uropa katika mchezo wao wa kwanza na Borussia Dortmund nchini Ujerumani ulioishia kwa sare ya 1-1.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji alifunga goli hilo kwa mpira wa krosi ya chini wakati Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akirejea kuvaana na klabu yake hiyo ya zamani ya Borussia Dortmund.

Katika mchezo huo kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller pia alimyima goli Origi akiwa amebakia yeye na kipa huyo. Dortmund ilipata bao lake la kusawazisha kupitia kwa Mats Hummels.
                            Divock Origi akifunga goli katika mchezo wao na Dortmund
         Kula tano Mwanangu: Kocha Jurgen Klopp akimpa mkono kumpongeza Origi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni