.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

KUISHI MIAKA ZAIDI YA MITANO JIJINI MWANZA BILA KUFIKA ENEO LA SAMAKI NI AJABU.

Mwananzengo Robert Kasamwa akifurahia ujio wa 102.5 Lake Fm katika eneo la Samaki Jijini Mwanza.

Imezoeleka kuona mtu yeyote akifika Jijini Mwanza, lazima akapige picha katika sanamu ya Samaki ililopo katikati ya Jiji, lakini kwangu imekuwa tofauti. Kama umefika hongera ila kama hujafika fanya hima ufike.

Nimeingia Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza mwaka 2011, lakini sikuwahi kuwa na wazo la kwenda kupiga picha katika eneo hilo. pengine mtanisaidia ni uzalendo uliniponyoka au ni nini haswa kilinizubaisha.

Katika kipindi chote hicho, sikuwahi kukanyaga eneo la Samaki licha ya kwamba kama si kila siku, basi japo mara moja kwa juma, nimekuwa nikipita katika eneo hilo na kujionea umati wa watu wakipiga picha.

Safari yangu ya miaka mingi kuwa Jijini Mwanza bila kukanyaga eneo la Samaki inahitimishwa Mwaka huu 2016, baada ya ujio wa 102.5 Lake Fm Mwanza, ambapo hatimae nimefika katika eneo hilo na kupiga picha na Wananzengo wenzangu. 

Hakika hayawi hayawi, hatimae yamekuwa. Japo kukaa zaidi ya miaka mitano Jijini Mwanza bila kufika eneo la Samaki ni ajabu.
Mtayarishaji wa Makala haya George Binagi-GB Pazzo akifurahia ujio wa 102.5 Lake Fm katika eneo la Samaki Jijini Mwanza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni