.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Aprili 2016

KUSANYIKO LA KUMUENZI MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA KUFANYIKA KESHO 30.04.2016, TRIPLE 7 KAWE

Ndugu zetu pamoja na Marafiki zetu, wakati huu tukiendelea kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushiriki wenu wa hali na mali katika kuandaa safari yake ya mwisho.Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya tarehe 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari
za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya
Milele.
Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe
Imetolewa na Dr. George Longopa
KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar ES SALAAM

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni