Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi waliopata majanga ya kuingiliwa na maji katika nyumba zao wakati alipotembelea kambi maalum iliowekwa katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere, alipofika kuwafariji na kuwapa pole na mtihani huo.
Baadhi ya Wananchi wa maeneo ya Nyerere, Kwahani Kwa Wazee na Sebleni wakiwa katika Kambi maalum ilioandaliwa kwa Wananchi waliopata maafa ya kuingiliwa na Maji Nyumba zao wakati wa mvua ilionyesha juzi jumapili katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji Wananchi waliopata maafa ya mvua katika baadhi ya maeneo ya Visiwa vya Unguja, Katika Kituo hicho kuna Wananchi zaidi ya mia nne waliopata maafa hayo wakiishi kwa muda katika kituo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsiliza Afisa wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayotowa huduma ya kwanza kwa Wananchi hao
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi msaada wa Vyakula vilivyotolewa na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Amaan Zanzibar, wakati alipofika katika Kambi hiyo kuwafariji Wananchi hao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni