Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba kwa pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wametembelea machinjio ya Vingunguti na kuona jinsi hali ilivyo katika eneo hilo.
Pamoja na kutembelea eneo hilo ambalo lilikuwa limefungiwa kuchinja nyama, mawaziri hao wameruhusu kwa siku tatu kuchinja huku wakitoa maagizo kwa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala kuhakikisha wanapafanyia marekebisho Mkaguzi toka TFDA Dkt. Mwanga Itikija (mwenye shati la pink) akiwaonesha mawaziri hao eneo ambalo lilikua likiuzia nyama kwa reja reja kinyume na kanuni ya afya. Mbunge wa jimbo la Segerea, Bona Kalua, akiongea na wanachama wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Ng'ombe na mazao yake (UWAMI) kwenye mkutano wa pamoja na mawaziri hao.
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Wanachama wa umoja huo, ambapo aliwasisitiza kufanya biashara kwa kuzingatia kanuni za afya na kumlinda mlaji hivyo kuwa makini na utunzaji wa mazingira pamoja na mazao wanayoyauza machinjioni hapo.
Waziri Mwigulu Nchemba akiongea na Umoja huo na kuwapatia siku tatu ili waendelee na uchinjaji wa ng'ombe walizonazo na baada ya hapo wataendelea na ukarabati wakati huo machinjio ya mazizini yatakua yamekamilisha ukarabati na kufunguliwa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilaya ambaye ndio Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto akiongea kwenye mkutano huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni