Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akifunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akimpatia cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD).
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alishiriki katika kufunga mafunzo ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuhimiza mijadala na mazungumzo kati ya sekta binafsi na serikali, yaliendeshwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam- Shule ya Boiashara (UDBS) na kudhaminiwa na mradi wa BEST-PPD.
Katika hotuba yake ya ufungaji, Kasesela alisisitiza sana suala la nidhamu ndio msingi wa kujenga sekta binafsi iliyo imara. Pia aliwaasa kupunguza utitiri wa jumuiya za sekta binafsini na kusema ni muhimu zikaungana na kujenga moja yenye nguvu.
Aliwashauri halmashauri zote kufungua dawati kwa ajili ya mijadala na sekta binafsi. " Bila sekta binafsi imara uchumi wa nchi hauwezi kukua, ni muhimu sekta binafsi ikaanza kuchukua nafasi stahiki ikiwemo kutekeleza majukumu mengine kwa niaba ya serikali mfano ukuaji wa michezo mabayo inahitaji uwekezaji ili serikali iondokane na kuwekeza, nchi kama Marekani hazina wizara ya michezo" alisema.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni