Papa Francis amewasili katika kambi iliyopo kwenye
kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu
kuingia mataifa ya Ulaya.
Kambi hiyo ya Moria inawakimbizi 3,000, ambao
baadhi yao wanakabiliwa na hatua za kurudishwa nchini Uturuki. Papa
Francis anatarajiwa kula mlo wa mchana na wakimbizi 250.
Papa Francis amesema safari yake ya Ugiriki ni ya
kushuhudia janga kubwa la wahamiaji duniani kutokea tangu vita ya
pili ya dunia. Papa Francis ameahidi kuwachukua wakimbizi 10.
Papa Francis akiongea na Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras baada ya kuwasili kisiwa cha Lesbos
Mkimbizi akiwa na bango la kumkaribisha Papa Franis katika kisiwa cha Lesbos
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni