.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 16 Aprili 2016

PAPA FRANCIS KWENDA KUWAUNGA MKONO WAHAMIAJI

Papa Francis anatarajiwa kutembelea kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kuuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kufika nchi za Ulaya.

Papa Francis ambaye atakutana na kiongozi wa Orthodox, Patriarch Bartholomew, atatembelea kambi ya watu zaidi ya 3,000 wanaongojea ama wapatiwe hifadhi ama warejeshwe Uturuki.

Kisiwa cha Lesbos kimekuwa ni eneo muhimu la kuingilia Ulaya kwa wahamiaji katika mwaka uliopita.
Maelfu sasa wamekwama katika kisiwa hicho baada ya mwezi uliopita Umoja wa Ulaya na Uturuki kuingia makubaliano ya kupunguza tatizo la wahamiaji.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni