Jumapili, 10 Aprili 2016
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASEMA MALARIA INAWEZA KUMALIZWA
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na mengine kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti hali ambayo imechangia sana katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji, Bw. Wolft Blitzer wa CNN.
Mwanzilishi wa Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya Sumitomo Chemical ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.
Sehemu ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria
Mhe Rais Mstaafu akiwa na Bw. Ray Chambers na Mkewe Bi. Patti Chambers muda mfupi kabla ya hafla ya kuanza.
Mhe Kikwete akiwa na Bw Blitzer mtangazaji maarufu wa CNN kupitia kipindi chake cha Situation Room
Mhe. Kikwete akiwa na sehemu ya wageni wakipata picha
Mhe Kikwete akiwa na ujumbe wake kutoka kushoto ni Bw. Togolan Mavula, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Professa Mohamed Janabi
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni