.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 10 Aprili 2016

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza jipya Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo la Mapinduzi kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7 na taasisi za wizara alizozivunja amezihamishia ambapo katika baadhi ya wizara za sasa.

Mawaziri hao watawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.

2). Wizara nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na utawala bora - 
Mhe. Haroun Ali Sleiman.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Katiba .Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Khamis Juma Maalim.

3). Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ - Mhe. Haji Omari Kheir.

4). Wizara ya nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais - Mhe. Mohammed Aboud. Mohammed

5). Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Dk. Khalid Salum Mohd.

6). Wizara ya Afya- Mhe Mahmoud Thabit Kombo.
Naibu Wizara ya Afya . Mhe.Harusi Said Suleiman.

7). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali- Mhe.Riziki Pembe Juma
Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali.- Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri.

8). Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Balozi Amina Salum Ali.

9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji- Mhe Balozi Ali Karume

Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji
Mhe.Mohamed Ahmed Salum.

10). Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo - Mhe.Rashid Ali Juma

Naibu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo.
Mhe.Chumu Kombo Khamis.

11).Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi- Mhe.Hamad Rashid Mohd

Naibu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
Mhe.Lulu Msham Juma.

12).Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.- Mhe.Mauldine Castiko.

13). Wizara ya Maji Ardhi Nishati na Mazingira - Mhe.Salama Aboud Talib.

Niabu Waziri Maji Ardhi Nishati na Mazingira.
Mhe.Juma Makungu Juma.

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, amewateuwa wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri wasio kuwa na Wizara Maalum

Mhe Said Soud Said - Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe Juma Ali Khatib -Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
Uteuzi huo umeaza leo tarehe 9/4/2016.

Waheshimiwa wanatarajiwa kuapishwa kesho Ikulu jumapili 10April 2016,Saa 3 asubuhi kwa ajili ya kuapishwa. Ikulu Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni