Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kisanga kitongoji cha Kiala akipokea taa ya kutumia mionzi ya jua kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela baada ya kupokea msaada huo kutoka wakala wa nishati vijini Rea.
Wakala wa Nishati Vijijini REA, wametoa msaada wa taa za kutumia mionzi ya jua katka kijiji cha Kisanga kitongoji cha Kiala Wilaya ya Iringa.
Kitongoji hiki ni kile kilichokumbwa na mafuriko na kaya zaidi ya 100 kukosa mahala pa kuishi. Kijiji kiliamua kuwatengea eneo ambalo watajenga makazi mapya.
Akitoa msaada huo, Bi Jaina Msuya Afisa habari REA aliwaasa wananchi kutunza taa hizo na kuhakikisha zinachukua muda mrefu.
Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya Iringa bwana Richard Kasesela alisema taa hizo zitasaidia kupunguza kutoa mwanga, pia watoto wanaweza kujisomea usiku na hatari ya nyoka itapungua.
REA wametoa taa zenye thamani ya tsh Mil 7. Wananchi wa kitongoji hicho wanaendelea na shughuli za ufyatuaji matofali ili kujenga nyumba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni