.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Aprili 2016

SHAKA ITAKA MIKOA YA KASKAZINI KUKATAA SIASA ZA UKANDA NA UZAWA

Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa SHAKA HAMDU SHAKA akabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga
Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anafungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang’a

kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwa wasili wilayani Mwanga
Katibu wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Yasin Lema akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya UVCCM wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro

                                                                                    Na Woinde Shizza, Mwanga


Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya
Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda
kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na
kujengeka katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba
kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike.

Hayo yamelezwa leo na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka
wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang’a kata
ya Mwanga mkoani hapa.

Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa
anaishi, kupigania madaraka., vyeo au utawala kwa kutumia maneno au sera
za ubaguzi wa dini, ukabila, uzawa au ukanda.

Aidha aliongeza kuwa baada ya miaka 52 ya uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika
na zanzibar, anapotokea kiiobgozi au chama cha siasa kinachokifanya
shughuli za kisiasa kwa kueneza sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa
ukanda ni hatari mpya mbele ya watanzania.

“Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna hatari inawanyemelea,
msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka kwake ni mbinde, ili
ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo si ajabu damu ikanwagika “alisema
Shaka

Alisema wakati baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo wakiaza kughilibiwa na
wanasiasa uchwara wakubali kuchagua vyana kwa sababu za ukanda na
ukabila, idadi kubwa ya wakaazi wa Mikao hiyo wanaishi na wamejijenga
kiuchumi katika mikoa mingine ya nchi na huko hawabughudhiwi wala
kubaguliwa.

“Haiikisha mkiendela kubagua wenzetu na nyinyi mtaanza
kubaguliwa,vdhambi ya ubaguzi haina toba, kataeni siasa chafu na
wakwepeni matapeli wa kisiasa na walafi wa madaraka “alisisitiza shaka.

Kaimu huyo katibu mkuu wa UVCCM alisema kwamba Taifa la Tanania
halikuachwa na wakoloni bali liliundwa na waasisi wake Marehemu baba wa
Taifa Mwalimu julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume bila na
kupiga vita ubaguzi wa kikabila, udini, rangi za watu au kuendekeza
uzawa.

Alisema kutendo chochote kitakachopelekea kuacha au kuipuuza misingi
ya Taifa letu ambayo imewafanya watu kuwa na umoja, upendo na
mshikamano radhi za waasisi hao pamoja na za wenzao zitaigeukia nchi
yetu iwapo tutakubali kugawanywa na wanasiasa wachovu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma
alisisitiza haja ya kuendelea kuheshimu na kudumisha umoja wa kitaifa
nchini na mwanasiasa yeyote atakayeonekaa kana ni mkabila, mdini na
asiyehimiza amani na utulivu aogopwe kama ebola.

“Ni mkoa upi leo hii nchini kwetu ambao wanaishi janii ya watu wa kabila
moja,dini moja,rangi moja au ukoo mmoja,tikate ukabila ns vyama
vilivyoanza kuonyesha ubaguzi wa aina yeyote “alisema Raibu

Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoani kilimanjaro alisema vyama vinavyopita na Nkueneza siasa za chuki, ukanda au ukabila vichunguzwe na ikiwa
vitatjibiiyika kujihusisha na vitendo hivyo hatari Msajili wa Vyama vya
siasa nchini achukue hatua za kisheria kuifuta mara moja kabla
havijaleta madhara.

Shaka na msafara wake wanaendelea na ziara katika wilaya ya Mwanga kabla ya kuhitimisha wilaya ya Same baadae kuelekea Mkoani Tanga.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni