Nahodha wa timu ya Uchukuzi SC,
Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa mchezo wa nusu fainali
dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mei Mosi,
Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni mkuu wa benchi,
Kenneth Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0.
Mwamuzi Robert Mkatakiu (aliyeshika
kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo Ally wa Tamisemi aliyelala
chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo alionyeshwa kadi hiyo pamoja na
nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia). Tamisemi walishinda kwa
magoli 2-0.
Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na
Tamisemi wakisubiri mpira wa kona upigwe na Omary Said wa Uchukuzi
(haonekani pichani). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Kipa wa Tamisemi,, Leonard Mkinga
(katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake kabla Uchukuzi
hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
Matalena Mhagama (GA) wa Uchukuzi SC
akijiandaa kufunga, pembeni ni Dora Njau (GD) wa TPDC. Uchukuzi
walishinda kwa magoli 33-14.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Uchukuzi SC na Tamisemi
kesho zitacheza mchezo wao wa mwisho wa netiboli, ambao ni kama
fainali kutokana na timu zote kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa
mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani
hapa, kila mmoja akiwa na pointi tisa.
Netiboli inachezwa kwa mtindo wa
ligi, ambapo timu hizo zinakamilisha ratiba na mmoja akimfunga
mwenzake atakuwa bingwa au zikitoka sare ya idadi yeyote ya magoli,
basi Tamisemi atatawazwa bingwa kwa kuwa anaidadi kubwa ya magoli ya
kufunga, 94 na wenzao wana 87.
Timu ya CDA Dodoma wanafuatia wakiwa
watatu baada ya kushinda mchezo mmoja, huku Tanesco na chipukizi wa
TPDC wakimaliza mashindano bila kushinda mchwezo wowote. Lakini TPDC
inayofundishwa na kocha mzoefu Rose Mkisi inayoundwa na wachezaji
wenye umri mdogo kati ya 20-30, ndio timu changa baada na inaonyesha
baada ya mwaka mmoja itakuwa tishio kwani itakuwa na uzoefu tofauti
na sasa ndio wameanza mwaka huu kushiriki mashindano haya ya Mei
Mosi.
Katika mchezo wa soka timu ya Geita
Gold Mine itakwaana na Tamisemi kesho katika mchezo wa fainali.
GGM wametinga hatua hiyo baada ya
kuwafunga Tanesco kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumaliza mchezo
wa nusu fainali bila kufungana.
Penati zote nne za GGM zilifungwa na
Gwetu Guvette, Oswald Binamungu, Ally Twist na Mohamed, wakati za
Tanesco walizopata ni Said Kondo na Stan Uhagile, na walizokosa ni
Hemed Mtumwa na Betwel Kagimbo.Nao Tamisemi waliwachapa Uchukuzi SC
kwa magoli 2-0.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa
jana jioni Uchukuzi SC waliwafunga chipukizi wa TPDC kwa magoli
33-14. Uchukuzi walikuwa mbele kwa magoli 15-8.
Nayo Tamisemi waliwapeleka jamaa zao
CDA na kuwachapa magoli 18-13. Washindi walikuwa mbele kwa magoli
9-8.
Katika kamba kwa wanaume Ukaguzi
waliwavuta CWT kwa mivuto 2-0, nayo TPDC wakiwavuta UDOM mivuto 2-0,
na Uchukuzi SC walipata ushindi wa chee baada ya Tanesco kuingia
mitini; wakati kwa wanawake Tamisemi waliwavuta bila huruma Tanesco
mivuto 2-0.
Mbali na netiboli na soka
itakayochezwa kesho, pia kutakuwa mechi za kamba wanaume TPDC kucheza
na CWT, huku UDOM kuumana na Tanesco; wakati wanaume Uchukuzi SC
watakutana na TPDC.
MWISHO
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni