.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 13 Aprili 2016

WANANCHI WA KATA YA MANG'OLA WALALAMIKIA KITENDO CHA MKUU WA WILAYA KUFUNGA SHUGHULI ZA UVUVI ZINAZOFANYWA NDANI YA ZIWA EYASI

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hiii leo wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliopo ndani ya wilaya ya karatu mkoani Arusha
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anajaza mchanga kwa ajili ya kufetua matofali hiii ikiwa nimoja ya mradi ambao ameutembelea katika kata hiyo
Diwani wakata ya mang'ola Lazaro Gege akiwa anampa maelezo kwa ufupi ya mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa
Mwenyekiti wa umoja wa  vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu mkuu wa vijana taifa
                         Baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo
                                                                                              Na Woinde Shizza,Karatu

Wananchi wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang’ola wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamikia kitendo cha serekali kufungia ziwa Eyasi na kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya vijana wengi kukosa kazi na kinaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukubwa na baa la njaa kutokana na kumaliza chakula chote ambacho walikuwa wamekiifazi kwa ajili ya chakula cha akiba akiba.

Hayo waliyasema leo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya miradi inayofanywa na chama pamoja na kuongea na wananchi wa kata hiyo.

Walisema kuwa wanasikitishwa sana na kitendo cha mkuu wa wawilaya kuwasimamisha shughuli zao za uvuvi kwani ndizo walizokuwa wakizitegemea katika kujipatia kipato pamoja na chakula katika kijiji hicho na kata kwa ujumla.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema kuwa tangu marchi 19 walizuiwakufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo hilo na kupewa masaa 24 kuondoka katika eneo hilo kwakile kilichodaiwa kuwa eneo hilo limekubwa na ugonjwa wa kipindu pindu.

“unajua mimi ni mfanya biashara nimetokea mbali nasio mimi tu tupo wengi naninavijana wangu ambao nimekuja nao hapa kwa ajili ya shughuli hii ya uvuvi sasa tarehe hiyo 19 mwezi wa tatu mkuu wawilaya alikuja apa na askari nakutupa masaa 24 tuwe tumeondoka kuhoji nini ni wakatuambia ni pachafu mara waseme kuna kipindu pindu tukawaambia kama ni pachafu watuache wakagoma wakasema tumesema muondoke ndiposisi kwa kuwa tunaogopa nakamaunavyojua wananchi tulivyo waoga tukaondoka na tulivyoondoka walituambia baada ya siku chache wangefungua lakini adi sasa apajafunguliwa tunateseka sana ata vyakula vyetu vya akiba tumemaliza yaani apa ni tabu tu”alisema Nyato

Kwa upande wa mwananchi mwingine aliejitambulisha kwa jina la Wiliam Jonas alisema kuwa mara baada ya ziwa hilo kufungwa wamekuwa wanaishi maisha ya kuomba omba ,wao kama wananchi wanagawana chakula walichokuwa wamekiifadhi na kinakaribia kwisha na vijana wengi walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo wamekuwa wazururaji.

Akiongea na wananchi hao Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa yeye kama katibu amesikia malalamiko yao naatayafanyia kazi kwa kukutana na mkuu wawilaya nakuona ni jinsi gani ambavyo wataweza kutatua tatizo hilo.

Gazeti hili halikuishia hapo ilibidi kumtafuta mkuu wa wilaya ya karatu Omary Kwaanq ili kuzungumzia tuhuma hizi nakusema kuwa kweli wamelifunga ziwa hilo kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeikumba wilaya yake .

Alisema kuwa mpaka sasa wilaya yake ina wagonjwa 70 wa kipindu pindu na wamefanya utafiti ukaonyesha wagonjwa wengi wametokea maeneo ya ziwa hilo.

“tumefanya utafiti kiukweli kwa kushirikina na mtaalamu wamagonjwa wa milipuko nakubaini kuwa maji yale ya ziwa yana chembe chembe za wadudu wanao eneza ugonjwa wa kipindu pindu hivyo tukaamua ni borakufunga ziwa ilo ili wananchi wasiendelee kuzurika na ugonjwa huo.

Aliongeza kuwa mara baada ya kuona maji yale ya ule mto yana vimelea vya ugonjwa wa kipindu pindu ndio maana wakaona ni bora wafunge ziwalile ili wananchi wasiendele kupata ugonjwa huo hatari.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni