.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Aprili 2016

WAZIRI KITWANGA APIGA MARUFUKU KUCHEZA "POOL TABLE" WAKATI WA KAZI JIMBONI KWAKE

POO1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na wananchi wa mji wa Misungwi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo hilo. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwaka wananchi hao kufanyakazi ili jimbo hilo lizidi kusonga mbele. Pia Mbunge huyo alipiga marufuku uchezaji wa pool table wakati wa kazi.
POO2
Mkazi wa Misungwi mjini, Songoro Msafiri (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia aliyekaa), mara baada ya Mbunge huyo kumaliza kuzungumza na wananchi hao na kuruhusu kuuliuzwa maswali mbalimbali yanayowakera jimboni humo. Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili waliletee maendeleo jimbo lao.
POO3
Wananchi wa mjini Misungwi wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini huo leo.
POO4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na mabalozi wa mashina wa CCM katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Wilaya ya Misungwi. Kitwanga aliwashukuru mabalozi hao kwa kumchagua na kuwaomba washirikiane zaidi ili kuliletea maendeleo jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.

 

                                                                                     Na Felix Mwagara, Misungwi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani Misungwi kuwakamata vijana watakaocheza mchezo wa pool wakati wa kazi jimboni humo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Misungwi na kuhudhuria na mamia ya wananchi wa mji huo, Kitwanga alisema wilaya hiyo inahitaji maendeleo na mabadiliko makubwa zaidi na mabadiliko hayo yanakuja kutokana na ufanyaji kazi. Aliserma kazi ndio msingi wa maendeleo hivyo ili maendeleo yapatikane lazima watu wafanyekazi katika maeneo yao.

“OCD (Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya) nisione na sitaki kusikia vijana wa Misungwi wanacheza pool asubuhi, nashangaa sana kwanini mnapenda pool, pool sio kazi, na maendeleo hayawezi yakaja kwa kucheza pool, chezeni jioni baada ya muda wa kazi,” alisema Kitwanga

Kitwanga aliwataka wananchi jimboni kwake kuanzisha vikundi ili waweze kupewa mikopo kupitia fedha alizoziahidi Rais John Magufuli kuwa atatoa kwa kila kijiji shilingi milioni hamsini.

“Fedha zipo jirani kuja, hivyo anzisheni vikundi ili muweze kukopeshwa fedha hizo na muweze kufanya mambo ya maendeleo, fedha hizo ni kwa ajili ya mikopo hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuanzisha vikundi vyenu ili muweze kuzipata fedha hizo kwa uharaka zaidi,” alisema Kitwanga.

Wakati huo huo, Mbunge huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kuhakikisha anawachukulia hatua kali wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi watakaoomba rushwa kwa wagonjwa au ndugu wa wagonjwa. Kitwanga alisema hayo baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu kukithiri kwa rushwa katika hospitali hiyo ya wilaya.

Hata hivyo, Waziri Kitwanga aliwahakikishia wananchi wa jimbo hilo wawe watulivu na wasubiri maendeleo, na pia waendelea kuchangia maendeleo ya jimbo lao ikiwemo uchangiaji wa madawati katika shule zao. Kuhusu barabara Kitwanga alisema barabara zote ambazo hazipitiki zitatengenezwa hivi karibuni na tatizo la maji litakuwa historia kwani mipango ya upatikanaji wa maji hayo ilishakamilika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni