.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Aprili 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KIKAZI IFAKARA, MOROGORO


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi katika hospitali ya Rufaa ya St. Francis pamoja na wajawazito wanaosubiri kujifungua na ambao wapo chini ya uangalizi wa madaktari.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya siku 1 mjini Ifakara kufuatilia utendaji wa shughuli mbalimbali za Afya Wilayani Kilombero, Morogoro.

Katika ziara hiyo, Mhe Ummy ambae alieambatana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe Florence Tonguely-Mattli alifungua kozi ya miezi mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kina mama wajawazito hususani katika eneo la upasuaji na utoaji wa dawa za usingizi.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH) chini ya Mradi wa "Upatikanaji wa Uzazi Salama Tanzania" yanawahusisha Washiriki 70 kutoka mikoa ya Morogoro, Njombe na Mbeya.

Mhe Ummy pia alikagua shughuli mbalimbali za taasisi za afya ikiwemo kutembelea Taasisi ya Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute), Hospitali Teule ya Rufaa ya St. Francis, Chuo cha Uunguzi cha Edgar Malanta na Chuo Kikuu cha Tiba cha St. Francis.
Mhe Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH) Prof. Pemba, Balozi wa Uswisi nchini Mhe Florence Tonguely-Mattli.

                                                                                                                 Picha ya pamoja.


Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na washiriki wakati wa kufungua mafunzo ya miezi mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kinamama wajawazito mjini katika taasisi ya TTCIF, Ifakara.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni