Waziri wa Uchukuzi wa Ubelgiji amejiuzulu kufuatia
tuhuma za kudharau mdororo wa usalama katika uwanja wa ndege wa
Brussels kabla ya mashambulizi ya Machi 22.
Vyama vya upinzani vimekuwa vikishinikiza waziri
huyo Bi. Jacqueline Galant ajiuzulu.
Wapinzani wamepata nyaraka za siri za Umoja wa
Ulaya za mwaka 2015, zilizokosoa hatua za kiusalama katika viwanja
vya ndege vya Ubelgiji.
Mashambulizi katika uwanja wa ndege wa Zaventem na
kwenye stesheni ya treni yaliyofanywa na kundi la Dola ya Kiislam
yaliuwa watu 32.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni