Muwania urais wa Marekani kwa chama
cha Republican Donald Trump sasa hana mpinzani ndani ya chama chake
baada ya mpinzani wake mkuu Ted Cruz kujitoa katika mbio za urais.
Cruz ametangaza kujitoa katika mbio
hizo baada ya kushindwa na mfanyabiashara Trump katika jimbo la
Indiana.
Trump, ambaye si maarufu sana ndani
ya chama chake, sasa njia ni nyeupe ya kuwania urais anachongojewa ni
kuidhinishwa na wajumbe 1,237 wa chama cha Republican.
Donald Trump akisalimiana kwa furaha na wafuasi wake
Ted Cruz akiongea wakati wa kutangaza kujitoa mbio za urais Marekani



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni