Mshambuliaji wa Chelsea, Diego
Costa, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania
kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016, wakati mabingwa hao watetezi
wakijiandaa kutetea kombe hilo.
Kocha Vicente del Bosque pia ameamua
kuwachukua wachezaji wengine wenye majina makubwa kama mshambuliaji
wa Atletico Madrid, Fernando Torres, kiungo wa Manchester United,
Juan Mata na nyota wa Arsenal, Santi Cazorla.
Katika kikosi chake cha wachezaji 25
kocha huyo amewaita Cesc Fabregas, Pedro, Cesar Azpilicueta, David
Silva pamoja na golikipa David de Gea ambao ni wachezaji wanaosakata
soko katika Ligi kuu ya Uingereza.
Juan Mata aliyetemwa kikosi cha taifa
Fernando Torres katemwa naye
Kikosi Kamili ni:-
Makipa: Iker Casillas (Porto), David
De Gea (Manchester United), Sergio Rico (Sevilla)
Mabeki: Jordi Alba, Gerard Pique,
Marc Bartra (all Barcelona), Sergio Ramos, Dani Carvajal (Real
Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Juanfran (Atletico Madrid)
Viungo: Sergio Busquets, Andres
Iniesta (both Barcelona), David Silva (Manchester City), Mikel San
Jose (Athletic Bilbao), Koke, Saul Niguez (both Atletico Madrid),
Cesc Fabregas (Chelsea), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Isco (Real
Madrid), Bruno Soriano (Villarreal)
Washambuliaji: Pedro Rodriguez
(Chelsea), Alvaro Morata (Juventus), Aritz Aduriz (Athletic Bilbao),
Nolito (Celta Vigo), Lucas Vazquez (Real Madrid).



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni