.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Mei 2016

KUMCHEZESHA MCHEZAJI ERASTO NYONI

Timu ya Azam FC ya Dar es Salaam, imenyang'anywa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu uliyoupata katika mechi Na. 156 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.

Uamuzi huo umetokana na Azam kumtumia mchezaji Erasto Nyoni kwenye mechi hiyo wakati akiwa na kadi tatu za njano. Mchezo huoulifanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake. Hivyo kwenda kinyume na Kanuni husika.

Pia kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.

Kadhalika Bodi ya Ligi imelionya Benchi la Ufundi la timu hiyo kuongeza umakini katika utunzaji wa kumbukumbu za kadi za wachezaji wake. Pia imezikaribisha timu zote wakati wowote kuomba kumbukumbu zozote kila zinapozihitajika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni